News RSS/Atom Viewer Classic
Sponsored Links
Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa amezitaka Israil na Palestina kufanya juhudi zaidi ili kuafikia mkataba wa amani katika eneo la Mashariki ya kati.
Serikali ya Ethiopia imekiri kuchukua hatua za kuzuia kituo cha radio cha Marekani, VOA, Kupeperusha matangazo yake nchini humo mbali na kubana matangazo yake.
Kiongozi wa chama cha upinzani kilichosajiliwa na serikali nchini Rwanda, ameondolewa kama kiongozi wa chama cha PS Imberakuri.
Aliyekuwa mjumbe wa Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan akiri kufanya mazungumzo na vigogo wa Taliban kwa muda wa mwaka mzima.
Nigeria imemwamuru balozi wake nchini Libya arejee nyumbani kufuatia matamshi ya rais Muammar Gaddafi, kupendekeza kugawanywa kwa taifa hilo.
Chama kikuu cha upinzani nchini Namibia, Rally for Democracy and Progress, RDP kimesema kitasusia sherehe za kuapishwa kwa wabunge baadaye hii leo.
Mahakama ya Kimataifa ya ICTR, imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa mbele yake dhidi ya hukumu ya kifungo cha miaka 15 iliyoitoa awali kwa mwimbaji Simon Bikindi.
Mahakama ya katiba nchini Togo, imethibitisha ushindi wa rais Faure Gnassingbe, kufuatia uchaguzi uliotawaliwa na mizozo mapema mwezi huu.
Mfalme Albert wa Pili wa Ubelgiji, atahudhuria sherehe za kuadhimisha miaka 50 tangu Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Congo, ilipojinyakulia uhuru wake.
Hatimaye timu zitakazopambana hatua ya robo fainali kuwania ubingwa wa vilabu vya Ulaya maarufu Champions League zimejulikana, huku Arsenal wakianza na Barcelona wakati Manchester United wataanzia ugenini Ujerumani wakichuana na Bayern Munich.
Kocha wa England Fabio Capello amemualika David Beckham kujiunga na kikosi cha England cha Kombe la Dunia nchini Afrika Kusini licha ya kiungo huyo kuwa ameumia.
Mshambuliaji wa Tottenham Jermain Defoe hatocheza soka kwa "wiki kadha" baada ya kuumia msihipa ya paja, kwa mujibu wa mejena wa timu Harry Redknapp.
Idhaa ya Kiswahili ya BBC inafanya vipindi mbali mbali vya kukumbuka miaka 20 tangu kifo cha hayati Luambo Makiadi, a.k.a Franco, mwanamuziki maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
BBC World News, katika mfululizo wa vipindi maalum vya televisheni na radio, vile vile online, wameanzisha shindano la kuandaa makala fupi ya video - iwe ni umeipiga kwa digital camera au mobile phone camera, ruksa!
Elimu kwa vijana kuhusu afya ya uzazi.
Magazeti na vyombo vya habari vya Afrika ya Mashariki.
Sofomo ™ © 2007