Mahakama ya Kimataifa ya ICTR, imetupilia mbali rufaa iliyowasilishwa mbele yake dhidi ya hukumu ya kifungo cha miaka 15 iliyoitoa awali kwa mwimbaji Simon Bikindi.
Shirika la kimataifa la msalaba mwekundu ICRC, limesema mfanyakazi wake aliyetekwa nyara miezi mitano iliyopita katika jimbo la Darfur ameachiliwa huru.
Baada ya mwezi mmoja tu wa kuchukuwa mamlaka ya uongozi kaimu Rais wa Nigeria Goodluck Jonathan ameanza kudhihirisha uwezo wake kwa kuvunja baraza la mawaziri.
Polisi wa Afrika Kusini wamewafyatulia risasi za mpira watoto wa shule waliokuwa wakiandamana kumlaani mwanamuziki mmoja aliyefikishwa mahakamani kwa mashtaka ya mauaji.
Uchunguzi umebainisha kuwa barani Afrika huchangia 4% ya hewa inayochafua mazingira pekee, licha ya kuwa bara ambalo limeadhirika zaidi na mabadiliko ya hali ya anga.
Shirika la Umoja wa Mataifa la makazi duniani, UN Habitat, limetoa ripoti inayozungumzia tabaka lililopo katika miji kwa wakazi wenye kipato kikubwa na wale walio na kipato duni.
Chama cha Soka cha Ghana (GFA) kimesema kinakusudia kumpata mchezaji wa zamani wa timu ya vijana wa umri wa miaka 21 ya Ujerumani Kevin Prince Boateng ili aichezee Black Stars.
Idhaa ya Kiswahili ya BBC inafanya vipindi mbali mbali vya kukumbuka miaka 20 tangu kifo cha hayati Luambo Makiadi, a.k.a Franco, mwanamuziki maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Waandishi wetu wa Uganda, Siraj Kalyango na Joshua Mmali walikuwa miongoni mwa waliofika eneo la Bududa mashariki mwa nchi hiyo ambako maporomoko ya udongo yalisababisha vifo vya mamia ya watu. Zifuatazo ni baadhi ya picha kutoka huko.