Serikali ya Marekani imetoa idhini kwa raia wake kuhama miji inayopakana na Mexico, baada ya makundi ya wafanyabiashara wa dawa za kulevya kuwaua raia watatu wa Marekani.
Raia wawili wa Ufaransa waliokuwa wameshikwa mateka wakiwa katika jamhuri ya afrika ya kati wameachiliwa huko Darfur na inaarifiwa kuwa wanaelekea Khartoum.
Aliyekuwa mke wa rais wa zamani wa Afrika Kusini, Nelson Mandela, Winnie Mandela, amekanusha kumtuhumu rais huyo wa zamani katika mahojiano na gazeti la Uingereza.
Baada ya taarifa za vyombo vya habari kuwa inasaidia serikali ya Somalia kijeshi, utawala wa mjini Washington umekanusha vikali taarifa hizo, na kusema hazina msingi.
Kaimu kiongozi wa Guinea, Jenerali Sékouba Konaté, amesema kuna maafisa wenzake wa kijeshi ambao wanapanga njama za kuipindua serikali ya sasa ya kijeshi.
Klabu ya soka ya Simba ya Dar es Salaam, Tanzania imenyakua ubingwa wa ligi kuu ya nchi hiyo, huku zikiwa zimesalia mechi mbili kabla ya kumaliza msimu.
Mchezaji matata wa Ivory Coast Didier Droga ameshinda tuzo la mwanasoka bora zaidi barani Afrika mwaka 2009 katika sherehe zilizofanyika mjini Accra Ghana.
Idhaa ya Kiswahili ya BBC inafanya vipindi mbali mbali vya kukumbuka miaka 20 tangu kifo cha hayati Luambo Makiadi, a.k.a Franco, mwanamuziki maarufu wa Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo.
Waandishi wetu wa Uganda, Siraj Kalyango na Joshua Mmali walikuwa miongoni mwa waliofika eneo la Bududa mashariki mwa nchi hiyo ambako maporomoko ya udongo yalisababisha vifo vya mamia ya watu. Zifuatazo ni baadhi ya picha kutoka huko.